Tanzania Coat of Arms
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE

Kliniki ya JKCI iliyopo SABASABA yaanza kutoa huduma kwa wananchi

  • Author: JKCI Admin
  • Published At: Sunday, Jun 28, 2026
image description

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kupitia kliniki yake iliyopo katika maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (SABASABA) yaanza kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wanaotembelea katika maonesho hayo.

Kupitia kliniki hiyo wananchi wanapimwa shinikizo la damu, sukari kwenye damu, mafuta kwenye damu, kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography), na kipimo cha kuangali mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiogram - ECG).

Vipimo vingine vinavyofanyika katika banda hilo ni vipimo vya maabara pamoja na kutoa chanjo ya homa ya ini. Aidha wananchi wanaotembelea banda la JKCI wanapata fursa ya kupata ushauri kuhusu lishe bora kutoka kwa wataalamu waliobobea katika lishe. 

Ili kuboresha afya za wananchi JKCI imepanga kutumia maonesho hayo kama sehemu ya kuongeza jitihada dhidi ya kinga ya magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo kutokana na magonjwa hayo kuongezeka na kupunguza nguvu kazi ya taifa.

Sambamba na kauli mbiu ya maonesho hayo JKCI imejipanga kuwa fahari ya Tanzania kupitia maonesho ya 50 ya SABASABA kwa kutoa huduma bora kwa kila mwananchi atakayetembelea banda hilo.