Tanzania Coat of Arms
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE
  1. Home
  2. All Publications

Publications

  • 1 download

    Mheshimiwa Dkt. Jafari Rajabu Seif, Naibu Waziri anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais, TAMISEMI,


    Dkt. Seif Shekalaghe Katibu Mkuu Wizara ya Afya,


    Ndugu Emanuel Tayari Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,


    Dkt. Grace Magembe Mganga Mkuu wa Serikali,

     

    Mheshimiwa Sixtus Mapunda Mkuu wa Wilaya ya Temeke,

     

    Ndugu Mavere Tukai, Mkurugenzi Mkuu wa MSD,


    Wakuu wa Taasisi chini ya Wizara ya Afya,


    Wakuu wa Idara na Vitengo wa MSD,

     

    Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya,


    Wafamasia wa Mikoa na Wilaya,


    Wageni Waalikwa,

    Waandishi wa Habari,


    Mabibi na Mabwana.

     

    KAZI NA UTU | TUNASONGA MBELE

     

    Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana hapa leo katika Ofisi za Bohari ya Dawa (MSD) kwa ajili ya tukio muhimu la kuzungumza na viongozi na watendaji wa Wizara ya Afya na OWM-TAMISEMI ili kuweka mikakati thabiti ya kuimarisha huduma ikiwemo uhakika wa upatikanaji wa bidhaa katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuimarisha afya za wananchi na kumpunguzia mwananchi mzigo wa gharama za matibabu. Lengo la kikao hiki ni kutoka na majawabu yatakayoimarisha  mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya nchini na kuongeza uwajibikaji wa sekta ya afya kwa umma nchini. 

     

    Napenda pia kutumia nafasi hii kuwashukuru wananchi wa Tanzania kwa kuendelea kuonyesha imani kubwa kwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Dkt, Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuboresha huduma za afya nchini. Ushiriki huo unaonekana wazi kupitia maoni, mapendekezo, na taarifa mbalimbali mnazotuma kupitia mifumo mbalimbali ikiwemo mfumo wa Ongea na Waziri wa Afya.

     

    Ndugu Wananchi, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka msisitizo mkubwa katika kuboresha huduma za jamii, hususan huduma za afya. Katika kutekeleza azma hiyo, Wizara ya Afya imeendelea kubuni na kuimarisha mifumo mbalimbali inayolenga kuhakikisha huduma za afya zinakuwa bora zaidi, zinapatikana kwa urahisi, na zinatolewa kwa kuzingatia haki na utu wa kila mwananchi.

     

    Lengo kuu la kikao kazi cha leo ni kuzungumza  kwa uwazi kuhusu upatikanaji wa awa nchini, kwa sababu ukweli ndiyo msingi wa uongozi wa haki na wa kujenga imani kwa wananchi. Tuzungumze kwa kufunguka kuhusu hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vipimo na bidhaa nyingine muhimu za afya katika nchi yetu. Ninaamini kwamba jamii inayothubutu kuzungumza wazi kuhusu changamoto zake ndiyo jamii inayoweza kupata majibu ya kudumu. Chini ya uongozi wangu Wizara ya Afya, uwazi si chaguo, bali ni msingi wa kutambua ukweli, kujifunza kutokana na mapungufu, na kuyatatua kwa maslahi mapana ya watu wetu.

     

    Kwanza kabisa, napenda kusisitiza jambo moja muhimu: Serikali inaendelea kuwekeza kwa nguvu kubwa katika sekta ya afya, hususan katika upatikanaji wa bidhaa muhimu za afya, na dhamira yake ni moja tu - kulinda maslahi ya wananchi. Serikali haipo kwa ajili ya jambo lingine lolote isipokuwa kuhakikisha mwananchi anapata huduma bora, salama, yenye uhakika na kwa wakati.

     

    Kwa mujibu wa tathmini iliyowasilishwa, ni kweli kwamba katika ngazi ya taarifa rasmi, upatikanaji wa dawa unaonekana kuwa juu, ukiwa karibu wastani wa asilimia 89 hadi 90. 

     

    Hii inaonesha kwamba Serikali imeweka mkazo mkubwa katika ununuzi, ugavi, usimamizi wa bohari, pamoja na kupeleka bidhaa hizi katika ngazi mbalimbali za huduma - zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, na mikoa, Hospitali za kanda, Hospitali maalum ya Taifa. Hii ni ishara kwamba uwekezaji wa Serikali unaonekana na una matokeo.

     

    Hata hivyo, ninatambua kwamba pamoja na takwimu zinazoonesha hali nzuri ya upatikanaji wa dawa, bado yapo malalamiko ya wananchi katika baadhi ya maeneo ya kutolea huduma. Hili linaonesha kuwa kuna tofauti kati ya picha inayojitokeza kwenye takwimu na uhalisia anaoukutana nao mwananchi anapofika kupata huduma. Takwimu zinaweza kuonesha uwepo wa dawa kwa ujumla, lakini bado zisiwe na tafsiri kamili ya upatikanaji halisi kwa wakati, mahali husika, na kwa kiwango kinachotosheleza mahitaji ya mgonjwa. Ndiyo maana Serikali hailitazami suala hili kwa juu juu. Tunalisikiliza kwa makini, tunalichukua kwa uzito mkubwa, na tunaendelea kulifanyia kazi kwa uwazi na kwa vitendo. Kwa sababu kulinda maslahi ya wananchi siyo kusimamia takwimu nzuri pekee, bali ni kuhakikisha huduma wanayoahidiwa inaonekana kweli katika maisha yao ya kila siku.

     

    Pale tunapoona kutokuwiana kati ya takwimu zinazotolewa na hali halisi ya utoaji wa huduma, tunao wajibu mkubwa wa kuhakikisha mambo hayo mawili yana fanana . Hatuwezi kuridhika na namba nzuri wakati mwananchi bado analalamika, na wala hatuwezi kupuuza malalamiko ya wananchi kwa sababu tu takwimu zinaonekana kuwa nzuri. Wajibu wetu ni kutafuta ukweli uliopo kati ya takwimu na uhalisia wa huduma, kubaini chanzo cha tofauti hiyo, na kuhakikisha kwamba taarifa tunazozitumia kufanya maamuzi zinaakisi hali halisi inayomgusa mwananchi. Hiyo ndiyo njia ya uongozi wenye uwajibikaji, na hiyo ndiyo njia ya kulinda maslahi ya wananchi.

     

    Katika kikao chetu cha leo cha tathmini ya hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya leo, yamebainika matatizo kadhaa ya ndani yanayoathiri ufanisi wa mfumo. Miongoni mwa matatizo hayo ni namna duni ya kuandika dawa, kushindwa kuagiza bidhaa kwa usahihi, usimamizi dhaifu wa stock, usimamizi dhaifu wa ndani katika vituo vya kutolea huduma, matumizi mabaya ya fedha zilizotengwa kwa bidhaa za afya, kutofuata ipasavyo kanuni za tiba na taratibu za ununuzi, pamoja na matumizi hafifu ya takwimu katika kutabiri mahitaji halisi ya bidhaa.

     

    Madhara ya tatizo hilo:

    Matatizo haya yamekuwa na madhara makubwa kwa wananchi na kwa mfumo mzima wa huduma za afya. Kwanza, yanasababisha dawa na bidhaa muhimu kutokuwepo kwa wakati au kuagizwa kwa kiwango kisichoendana na mahitaji halisi ya wagonjwa. 

    Pili, huongeza hatari ya kuisha kwa stock mapema au kuwepo kwa bidhaa zisizohitajika kwa kiwango kikubwa. Tatu, husababisha matumizi yasiyo sahihi ya rasilimali chache za fedha, jambo linaloongeza upotevu na kuzidisha shinikizo la kifedha kwenye vituo na taasisi za ugavi. Nne, hali hii hupunguza uaminifu wa wananchi kwa huduma za afya wanazopaswa kuzipata serikalini, kwa sababu taarifa rasmi zinaweza kuonesha upatikanaji, lakini mgonjwa akakosa huduma katika eneo la kutolea huduma. Mwisho, matatizo haya hudhoofisha uwezo wa Serikali kupanga kwa usahihi, kujibu mahitaji ya wananchi kwa wakati, na kufikia lengo la kuhakikisha upatikanaji endelevu wa bidhaa za afya kwa wote.  Hata hivyo, kuna mambo machache ninaomba niyaongelee kwa kina.

     

    Suala la maduka ya dawa ndani ya vituo vya afya lazima lishughulikiwe kwa umakini mkubwa  na kwa ujasiri wa kuukabili ukweli kama ulivyo:

     

    Maduka haya hayakuanzishwa kwa bahati mbaya. Hayakuletwa kwa lengo la kuongeza mzigo kwa mwananchi. Yaliwekwa kwa makusudi kabisa kama hatua ya kusaidia upatikanaji wa dawa pale ambapo mfumo wa kawaida wa ugavi ulikuwa haukidhi mahitaji ipasavyo. 

    Dhamira yake ilikuwa njema: kumsaidia mgonjwa apate dawa karibu na eneo la huduma, kupunguza usumbufu wa kwenda kutafuta dawa nje ya kituo, na kuziba mapengo yaliyokuwa yanaonekana katika upatikanaji wa bidhaa za afya.

     

    Kwa hiyo, hatukuweka maduka haya ili yawe sehemu ya tatizo; tuliyaweka yawe sehemu ya suluhisho. Na kwa sababu hiyo, haiwezekani, wala haikubaliki, kwa chombo tulichokibuni sisi wenyewe kwa nia ya kuboresha huduma, kugeuka baadaye na kuwa chanzo cha kuvuruga huduma, kuongeza malalamiko, kuchanganya wananchi, au kudhoofisha imani ya watu kwa mfumo wa afya wa umma.  Hata hivyo, hoja na mjadala uliowasilishwa vinaonyesha kwamba katika baadhi ya maeneo, utekelezaji wa mfumo huu una changamoto kubwa zinazohitaji kuchunguzwa na kurekebishwa bila kuchelewa. Katika baadhi ya vituo, maduka haya hayajaonekana kuleta tofauti ya haraka na ya moja kwa moja kwa mgonjwa, kwa sababu mchakato wa upatikanaji wa dawa bado unafuata mlolongo huohuo wa kawaida wa manunuzi, wenye taratibu ndefu na ucheleweshaji uleule. Matokeo yake, mgonjwa haoni tofauti kati ya huduma ya kawaida na huduma inayotolewa kupitia mfumo huu, ilhali matarajio yalikuwa kuona nafuu ya upatikanaji.

    Lakini jambo linalotia wasiwasi mkubwa zaidi ni malalamiko kwamba katika baadhi ya maeneo, dawa au bidhaa za afya ambazo zilipaswa kutolewa kwa wananchi  bure kupitia utaratibu wa kawaida wa huduma ya umma  kuhamishiwa kwenye maduka haya, na hivyo kumfanya mwananchi alazimike kununua kile ambacho kwa matarajio ya kawaida alipaswa kukipata bure ndani ya mfumo wa huduma wa umma. Kama jambo hili linatokea, hata katika maeneo machache, basi ni jambo zito sana. Hilo si tatizo dogo la kiutendaji; hilo linapingana na dhamira ya mfumo wenyewe. Ni kugeuza suluhisho kuwa tatizo. Ni kuharibu lengo la sera kwa vitendo vya utekelezaji. Na hili halikubaliki hata kidogo.

     

    Hatuezi tukarushusu mfumo tulioubuni kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa dawa ugeuke kuwa sababu ya usumbufu wa huduma. Hatutaruhusu kilichoundwa kusaidia wagonjwa kianze kuwakwamisha wagonjwa. Huo utakuwa ni mkanganyiko wa kimfumo ambao haupaswi kupewa nafasi ya kuendelea.

     

    Kituo cha afya cha umma si sehemu ya kufanya biashara kwa kutumia udhaifu wa mfumo wa ugavi. Haki ya mwananchi kupata huduma haiwezi kuathiriwa na tafsiri potofu ya uendeshaji wa maduka ya dawa ndani ya vituo. 

    Mwananchi hapaswi kufikishwa mahali pa kuamini kwamba dawa za kawaida za huduma ya umma zinapatikana tu kwa malipo kupitia utaratibu ambao awali uliwekwa kama nyenzo ya kusaidia. Hilo likitokea, maana yake ni kwamba tumetengeneza kwa mikono yetu wenyewe chanzo kipya cha kuvuruga huduma, kuongeza malalamiko, na kudhoofisha taswira ya serikali mbele ya wananchi.

     

    Kwa msingi huo, kama maduka haya katika hali ya sasa yanaongeza malalamiko, yanazalisha mkanganyiko wa utoaji huduma, yanadhoofisha dhana ya huduma ya umma, au yanapeleka ujumbe kwamba mgonjwa atalazimika kununua kile alichotarajia kupata ndani ya mfumo wa kawaida, basi ni wajibu wetu kuyapitia upya kwa kina. Mapitio hayo lazima yaangalie madhumuni ya awali, namna ya uendeshaji, vyanzo vya mtaji, taratibu za ununuzi, usimamizi wa mapato, ulinzi wa dawa za huduma ya umma, na athari halisi kwa mgonjwa. Na pale itakapobainika kwamba kuna upotovu wa dhamira, basi marekebisho yafanyike mara moja bila kusitasita.

     

    Kwa kifupi, msimamo wetu unapaswa kuwa huu: kile tulichokianzisha sisi wenyewe ili kuboresha huduma hakiwezi kuruhusiwa kuwa chanzo cha kuvuruga huduma. Kama mfumo wa maduka ya dawa ndani ya vituo vya afya bado ni wa manufaa, basi uthibitishwe kwa matokeo. Na kama utekelezaji wake umeanza kupingana na lengo lake, basi urekebishwe haraka ili urudi kuwa sehemu ya suluhisho, si sehemu ya tatizo.

     

    Tatizo lingine, Katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya, changamoto inayojitokeza si upatikanaji wa dawa kutokuwepo kabisa, bali ni kutokuwepo kwa uwiano kati ya dawa iliyopo kwenye kituo na dawa inayoandikwa na mtoa huduma. Mara nyingi, kituo kinaweza kuwa na dawa yenye kiambato tiba kilekile, ubora unaokubalika, na ufanisi unaokidhi mahitaji ya mgonjwa, lakini mgonjwa akaandikiwa jina la brand tofauti ambalo halipo kwenye stock ya kituo husika. Hali hii husababisha mgonjwa kupewa taarifa kuwa dawa haipo, wakati kiuhalisia dawa inayohitajika kwa madhumuni ya tiba ipo, isipokuwa imeandikwa kwa jina la kibiashara lisilopatikana katika kituo.

    Kwa mtazamo wa kisera na kiutawala, hali hii inaashiria tatizo katika uzingatiaji wa miongozo ya matumizi sahihi ya dawa, udhaifu wa uratibu kati wa huduma za tiba na huduma za famasia, pamoja na dosari katika usimamizi wa rasilimali za dawa ndani ya vituo. Aidha, pale ambapo mazoea haya yanafanyika kwa kuzingatia upendeleo wa brand fulani badala ya maslahi ya mgonjwa na uhalisia wa stock iliyopo, yanazua taswira ya ukiukwaji wa maadili ya utumishi, matumizi yasiyo sahihi ya mamlaka ya kitaaluma, na uwezekano wa kuwepo kwa maslahi binafsi yanayoathiri utoaji wa huduma.

     

    Ni muhimu kusisitiza kuwa uandishi wa dawa unapaswa kuzingatia jina la kitalaamu la dawa (generic name), miongozo ya tiba iliyopo, pamoja na dawa halisi zinazopatikana katika kituo husika. Mfumo wa utoaji huduma haupaswi kuendeshwa kwa kutegemea majina ya biashara pekee, hususan pale ambapo kuna dawa mbadala yenye kiambato kilekile na ubora unaokubalika kitaalamu. Kutofanya hivyo kunachochea malalamiko yasiyo ya lazima, huongeza usumbufu kwa wagonjwa, hupunguza ufanisi wa huduma, na hudhoofisha imani ya wananchi kwa mfumo wa afya.

     

     

    Kwa hiyo, suala hili linapaswa kutazamwa kama eneo muhimu la maboresho ya kiutawala na kitaalamu. Kunahitajika msisitizo wa utekelezaji wa sera ya uandishi wa dawa kwa majina ya generic, uimarishaji wa usimamizi wa ndani, ufuatiliaji wa mwenendo wa waandikaji wa dawa, pamoja na hatua stahiki pale itakapobainika kuwa kuna maamuzi yanayofanywa nje ya misingi ya kitaaluma au kwa maslahi binafsi. Lengo kuu linapaswa kuwa moja: kuhakikisha mgonjwa anapata dawa sahihi, kwa wakati sahihi, na kwa utaratibu unaozingatia weledi, uwajibikaji, na maslahi ya umma.

     

    Kwa hali hiyo, ni wajibu wa uongozi wa vituo na mamlaka husika kuhakikisha (DMO.RMO.CMO) kuwa mianya ya aina hii inafungwa, mifumo ya uratibu kati ya watoa huduma na famasia inaimarishwa, na kwamba maamuzi yote ya kitabibu yanabaki kuwa ya kitaaluma, ya haki, na yanayolenga ustawi wa mgonjwa. Hili si eneo la kuachwa liendelee kwa mazoea, bali ni jambo la msingi linalohitaji msimamo wa wazi wa kiutawala na hatua za maboresho ya mfumo.

     

    Suala la madeni kwa MSD lazima lisemwe wazi na lichukuliwe kwa uzito unaostahili:

    Madeni yamekuwa mzigo mkubwa unaokandamiza mfumo mzima wa ugavi wa dawa na bidhaa za afya. Hatuwezi kutegemea MSD iwe na uwezo wa kuagiza, kuhifadhi, na kusambaza dawa kwa wakati, wakati fedha zinazotokana na huduma zilizokwisha kutolewa hazirejeshwi kwa nidhamu na kwa wakati unaotakiwa. Ukweli ni huu: madeni ya vituo vya afya na hospitali kwa MSD sasa yanadhoofisha uwezo wa mfumo mzima kujikimu na kuwahudumia wananchi kwa uhakika. 

     

    Ni lazima tuelewane jambo moja. Mfumo wa ugavi wa dawa hauwezi kuwa imara kama fedha zinazopaswa kuzunguka ndani yake hazizunguki. Huwezi kuwa na mfuko unaozunguka kama fedha zinazotakiwa kurejeshwa hazirejeshwi. Huwezi kutaka dawa zipatikane kwa wakati wakati nidhamu ya matumizi ni dhaifu. Huwezi kutegemea ugavi uwe thabiti kama Taasisi zinachukua dawa, zinatoa huduma, lakini hazilipi madeni yake kwa wakati. Haya ndiyo yanayokwamisha uwezo wa MSD kutekeleza wajibu wake kikamilifu. 

    Kwa hiyo, ni lazima nitoe wito wa wazi kwa vituo vyote vya afya na hospitali zote nchini: lipeni madeni yenu kwa MSD. Huu si ushauri wa kawaida. Hili ni jukumu. Kila Taasisi inayodai huduma bora za ugavi lazima ionyeshe wajibu wake kwa kulipa madeni yake kwa wakati.  Na ninaposema hospitali zote, namaanisha zote - si hospitali ndogo tu, bali hata hospitali kubwa na za kitaifa pia. Hospitali kubwa nazo lazima ziwe mfano wa nidhamu ya kifedha. 

     

    Muhimbili National Hospital, MOI, JKCI, pamoja na hospitali nyingine zote za ngazi ya juu, lazima zitambue kwamba ukubwa wao hauwapi nafasi ya kuwa sehemu ya tatizo. Kinyume chake, ukubwa wao unawapa wajibu mkubwa zaidi wa kuwa sehemu ya suluhisho. Kama Taasisi kubwa zinaendelea kuwa na madeni makubwa yasiyolipwa kwa MSD, basi zinatuma ujumbe mbaya kwa mfumo mzima, na zinadhoofisha uwezo wa MSD kuwahudumia wengine pia. Tusijifiche nyuma ya hadhi ya Taasisi. Tusijifiche nyuma ya ukubwa wa hospitali. Wajibu ni uleule. Kama dawa zimechukuliwa, kama huduma zimetolewa, kama mapato yamepatikana, basi madeni yanapaswa kulipwa. Hakuna sababu ya taasisi inayopaswa kuwa kinara wa huduma za kibingwa na ubora wa usimamizi kuwa kinara wa madeni yasiyolipwa.

     

    Lazima tukubali kwamba bila nidhamu ya kifedha, upatikanaji wa dawa utaendelea kuyumba. Bila ulipaji wa madeni, MSD itaendelea kuwa na mzigo mkubwa wa kifedha. Bila kurejesha fedha kwenye mzunguko, tutazidi kuona ucheleweshaji wa ugavi, upungufu wa stock, na malalamiko ya wananchi. Na hali hii haiwezi kuendelea kuvumiliwa.

     

    Kwa hiyo, maelekezo yetu yanapaswa kuwa wazi:Kila hospitali, kila taasisi, na kila kituo chenye deni kwa MSD kitoe mpango wa kulipa deni hilo na kianze utekelezaji mara moja.Hospitali kubwa, zikiwemo Muhimbili National Hospital, MOI, na JKCI, zionyeshe mfano wa uwajibikaji kwa kulipa madeni yao na kurejesha nidhamu katika mfumo wa ugavi.  Fedha za dawa zilindwe, zikusanywe ipasavyo, na zirejeshwe kwa matumizi yaliyokusudiwa ili mfumo uweze kuendelea kufanya kazi.

     

    Kwa kifupi, hatuwezi kuzungumzia upatikanaji wa dawa bila kuzungumzia wajibu wa kulipa madeni kwa MSD. Hatuwezi kuitaka MSD ifanye miujiza wakati taasisi zinazopaswa kuilipa hazitekelezi wajibu wao. Wakati umefika wa kila ngazi kubeba wajibu wake. Kulipa deni kwa MSD si hiari; ni msingi wa kuokoa mfumo wa ugavi wa dawa nchini.

    Katika malalamiko haya ya ukosefu wa dawa, imejitokeza wazi kwamba picha ya hali halisi haitofautiani tu kutoka eneo moja kwenda jingine, bali pia inaonyesha jambo kubwa zaidi: suala la upatikanaji wa dawa haliamuliwi na miongozo, taratibu, au vipimo peke yake. Linategemea kwa kiwango kikubwa uimara wa menejimenti ya vituo vya kutolea huduma, ubora wa usimamizi wa ndani, na uwajibikaji wa viongozi katika ngazi zote.

     

    Mazungumzo yetu yameonyesha jambo la msingi sana. Mahali ambapo kuna uongozi thabiti, wenye mshikamano wa ndani, unaoshirikiana na wananchi, unaosimamia rasilimali kwa karibu, na unaoweka mbele maslahi ya umma, malalamiko ya ukosefu wa dawa hupungua au hutoweka kabisa. Katika maeneo hayo, dawa zinazopokelewa zinasimamiwa vizuri, taarifa za stock zinafuatiliwa, matumizi yanaangaliwa, na wananchi hupatiwa dawa wanazoandikiwa na wataalamu wao kwa wakati unaostahili.

     

    Lakini mahali ambapo menejimenti ni dhaifu, usimamizi ni hafifu, na uwajibikaji ni mdogo, ndipo tunapoanza kuona malalamiko ya mara kwa mara, kutokuwepo kwa mawasiliano mazuri kati ya kitengo cha tiba, famasia, stoo na utawala, pamoja na matumizi yasiyo sahihi ya dawa na rasilimali nyingine za afya. Hivyo basi, tunapaswa kukubali kwamba changamoto ya dawa siyo tu ya ugavi; pia ni changamoto ya uongozi, usimamizi, na nidhamu ya utekelezaji.

    Kwa msingi huo, ninaelekeza kwamba wafamasia washirikishwe kikamilifu katika menejimenti za hospitali, vituo vya afya, na zahanati. Haiwezekani tena sekta ya dawa, usimamizi wa stock, matumizi ya dawa, na ushauri wa kitaalamu kuhusu upatikanaji wa dawa vikabaki pembeni ya maamuzi ya kiutawala ya vituo. Mfamasia si mtu wa stoo pekee. Mfamasia ni mhimili wa usimamizi wa dawa, matumizi yake sahihi, ufuatiliaji wa stock, ushauri wa kitaalamu kwa uongozi, na udhibiti wa matumizi yasiyo sahihi ya dawa. Kwa hiyo, katika ngazi zote za utoaji huduma, wafamasia wanapaswa kuwa sehemu ya timu ya menejimenti na ya maamuzi, ili sauti ya kitaalamu kuhusu dawa isisikike pembeni bali iwe katikati ya uongozi wa kituo.

     

    Aidha, ninaelekeza pia kwamba Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, pamoja na Kamati zao za Ulinzi na Usalama, washiriki kikamilifu katika kusimamia upokeaji wa dawa na matumizi yake katika maeneo yao. Dawa zinapofika, zisipokelewe kama mzigo wa kawaida usiofuatiliwa. Upokeaji wake lazima usimamiwe kwa umakini, kwa uwazi, na kwa uthibitisho wa kutosha kwamba kilichotumwa ndicho kilichopokelewa, kimehifadhiwa ipasavyo, na kimeingizwa katika mfumo wa huduma kama ilivyokusudiwa.

    Lakini usimamizi usiishie kwenye kupokea tu. Ni lazima pia kusimamia matumizi ya dawa hizo ili kuhakikisha zinatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa. Haturuhusu dawa zilizopokelewa kwa ajili ya huduma ya wananchi zigeuzwe matumizi, zichepushwe, zifichwe, zitumike nje ya utaratibu, au zisitumike kwa walengwa waliokusudiwa. Kamati za Ulinzi na Usalama katika ngazi ya mkoa na wilaya zinapaswa kuona hili kama sehemu ya wajibu wao wa kulinda maslahi ya wananchi, kwa sababu suala la dawa si suala la kiutawala tu; ni suala la huduma, uhai wa wananchi, na imani ya umma kwa serikali yao.

     

    Kwa hiyo, tunataka kuona mnyororo mzima wa uwajibikaji ukifanya kazi: kutoka MSD na mfumo wa ugavi, hadi uongozi wa vituo, hadi ushiriki wa mfamasia katika menejimenti, hadi usimamizi wa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, na Kamati zao za Ulinzi na Usalama. Tukifanya hivyo kwa umakini, tutapunguza mianya ya upotevu, tutadhibiti matumizi mabaya, na tutahakikisha dawa zinazofika zinatumika kama zilivyokusudiwa - kwa kuwahudumia wananchi, si vinginevyo.

    Kwa kifupi, upatikanaji wa dawa haujengwi na mwongozo pekee, unajengwa na uongozi thabiti, menejimenti imara, ushiriki wa wataalamu sahihi, na usimamizi wa karibu wa matumizi ya dawa hadi kwa mlengwa. Pale ambapo haya yapo, malalamiko hupungua. Pale ambapo haya hayapo, malalamiko huongezeka. Na ndiyo maana sasa tunataka kila ngazi ibebe wajibu wake kikamilifu.

     

    Mkakati wa Wizar awa kupambana na hili tatizo, tunampango gani? Tunamalizaje au kupunguza tatizo?

    Katika kuimarisha upatikanaji wa dawa, usahihi wa uandishi wa dawa, na uwajibikaji katika utoaji wa huduma, Wizara tumeanza mchakato wa kutekeleza mfumo utoaji dawa kwa njia ya kielektroniki -                        e-Prescription - katika ngazi mbalimbali za utoaji huduma. Hatua hii inalenga kujenga mfumo wa kisasa, wenye uwazi na ufuatiliaji wa karibu, ambao utaunganisha huduma za kliniki, famasia, stock, na takwimu za matumizi ya dawa.

     

     

    Kupitia mchakato huu ambao tayari umeanza, tunalenga kushughulikia kwa njia ya kimfumo changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika vituo vya kutolea huduma; ikiwemo kuandika dawa ambazo hazipo kwenye stock, kuandika kwa majina ya brand badala ya generic names, kutokuwepo kwa ulinganifu kati ya huduma ya kliniki na famasia, pamoja na matumizi hafifu ya takwimu katika kupanga mahitaji. Mfumo huu utamwezesha mtoa huduma kuona kwa wakati halisi dawa iliyopo kwenye kituo, mbadala uliopo, na hivyo kuandika dawa kwa kuzingatia uhalisia wa stock na miongozo ya tiba.

     

    Kwa kuanza mchakato huu wa utekelezaji, tunaweka msingi wa kutatua matatizo mengi ya ndani ya mfumo wetu wa dawa na huduma. Kwanza, mfumo huu utasaidia kuimarisha nidhamu ya uandishi wa dawa kwa kuhakikisha kwamba dawa zinazoandikwa zinaendana na zile zilizopo au mbadala unaokubalika kitaalamu. Hii itapunguza hali ya mgonjwa kuandikiwa dawa ambayo haiwezi kupatikana ndani ya kituo, wakati dawa yenye kiambato kilekile ipo kwa jina tofauti.

    Pili, mfumo huu utasaidia kuimarisha matumizi ya majina ya generic katika uandishi wa dawa na kupunguza utegemezi wa majina ya biashara ambayo mara nyingi huwa chanzo cha mkanganyiko na malalamiko yasiyo ya lazima. Mgonjwa anahitaji tiba sahihi, si lazima brand fulani. Ndiyo maana mfumo huu utasaidia kuhakikisha kuwa maamuzi ya kitabibu yanaendana na dawa iliyopo na inayofaa kutumika.

     

    Tatu, tumeanza mchakato huu kwa kuelewa kwamba e-Prescription si suala la teknolojia pekee. Ni hatua ya kuunganisha kwa karibu zaidi kitengo cha tiba, famasia, stoo, na timu za uagizaji, ili dawa inapoandikwa, taarifa zake ziwe sehemu ya mkondo mmoja wa huduma na usimamizi. Hii itasaidia kupunguza pengo ambalo limekuwa likijitokeza kati ya wanaoandika dawa, wanaosimamia stock, na wanaopanga mahitaji.

     

    Nne, mfumo huu utatupa takwimu sahihi na za moja kwa moja kuhusu dawa zinazoandikwa, dawa zinazotolewa, dawa zinazokosekana mara kwa mara, na mwenendo wa matumizi katika kila ngazi ya huduma. 

    Takwimu hizi zitatusaidia kuboresha utabiri wa mahitaji, upangaji wa bajeti, uagizaji wa dawa, na ufuatiliaji wa utendaji wa vituo. Kwa hiyo, tunapoanza kutekeleza mfumo huu, tunaanza pia kujenga utamaduni wa kufanya maamuzi kwa kutumia ushahidi wa takwimu sahihi.

     

    Tano, utekelezaji wa e-Prescription utaongeza uwajibikaji katika kila hatua ya utoaji wa dawa. Itakuwa rahisi kufuatilia nani ameandika dawa, ameandika nini, kwa wakati gani, kwa kuzingatia stock ipi, na mgonjwa amepewa nini. Hii itasaidia kudhibiti uandishi usiofuata miongozo, upendeleo wa brand usio wa lazima, na matumizi yasiyo sahihi ya dawa.

     

    Kwa hiyo, tumeanza mchakato wa kutekeleza e-Prescription kwa sababu tunaamini kuwa huu ni mwelekeo sahihi wa kurekebisha mfumo wa usimamizi wa dawa nchini. Hatua hii haitabadilisha tu namna ya kuandika dawa, bali itasaidia kuleta nidhamu, uwazi, ufanisi, na usahihi katika mnyororo mzima wa huduma—kuanzia kwa mtoa huduma, famasia, stoo, hadi kwenye upangaji wa mahitaji na usimamizi wa kitaifa.

    Kwa kifupi, tumeanza mchakato huu kwa lengo la kuhakikisha kwamba mfumo wa utoaji wa dawa unakuwa wa kisasa zaidi, wenye uwazi zaidi, na unaojibu changamoto halisi zinazowakabili wananchi. Tunaamini kuwa utekelezaji wa e-Prescription utakuwa sehemu muhimu ya suluhisho la changamoto nyingi tulizonazo leo katika upatikanaji, matumizi, na usimamizi wa dawa.

     

    Ninapomalizia:

    Hatutaki tena maelezo mengi bila matokeo. Hatutaki tena takwimu nzuri kwenye karatasi wakati mwananchi bado anahangaika kupata dawa. Wakati umefika wa kila mmoja kubeba wajibu wake.

     

    Kwa hiyo, naelekeza yafuatayo:-

    Kwanza,Mfamasia Mkuu wa Serikali afanye mara moja uhuishaji wa formula ya kukokotoa hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya, ili kipimo hicho kisibaki kuonyesha uwepo wa dawa pekee, bali kizingatie pia utoshelevu wa dawa zinazopimwa sambamba na uhalisia wa orodha ya dawa zinazopaswa kupimwa katika kila ngazi ya utoaji huduma. Hatuwezi kuendelea kujiridhisha na kipimo kinachotoa picha nzuri ya takwimu wakati huduma halisi ina mapungufu.

    Pili,Mganga Mkuu wa Serikali asimamie kwa ukamilifu suala la uandishi wa dawa kwa kuzingatia Mwongozo wa Matibabu na Orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu. Sambamba na hilo, aongeze nguvu katika kuimarisha utendaji wa Kamati za Tiba na Dawa (MTC) ili zisiwepo kwa jina tu, bali zifanye kazi ya kusimamia matumizi sahihi ya dawa, nidhamu ya uandishi wa dawa, na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miongozo katika vituo vya kutolea huduma.

     

    Tatu,miongozo, miundo, na taratibu za usimamizi wa vituo vya kutolea huduma ipitiwe na kuboreshwa ili wafamasia wawe sehemu ya menejimenti ya hospitali, vituo vya afya, na zahanati. Haiwezekani masuala ya dawa, stock, matumizi ya dawa, na usimamizi wa bidhaa za afya yaachwe pembeni halafu tutegemee maamuzi ya menejimenti yawe sahihi na yenye tija. Wafamasia si watunzaji wa store pekee; ni wataalamu wa msingi katika upatikanaji, matumizi sahihi, usimamizi wa stock, na ushauri wa kitaalamu juu ya dawa. Kwa hiyo, miongozo ibadilishwe ili sauti ya mfamasia iwe sehemu ya maamuzi ya menejimenti, siyo sauti ya pembeni.

    Nne, vituo vyote na hospitali zote zenye madeni kwa MSD zikakae na MSD mara moja na kuandaa mpango mahsusi wa ulipaji wa madeni hayo. Nataka taarifa ya makubaliano hayo pamoja na mwanzo wa utekelezaji wa mpango huo niipate ndani ya miezi mitatu.  Ni lazima kila taasisi itambue kuwa kulipa deni kwa MSD si hiari; ni msingi wa kuimarisha mzunguko wa ugavi wa dawa nchini.

     

    Tano,Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri wasimamie kwa karibu na kwa umakini mkubwa matumizi ya fedha katika vituo vya kutolea huduma, ili yaendane na miongozo iliyopo, hususan katika ununuzi wa dawa na bidhaa za afya. Vilevile, wahakikishe matumizi sahihi na ya lazima ya mifumo ya taarifa na habari, kwa sababu bila taarifa sahihi hatuwezi kupanga kwa usahihi, kufuatilia kwa usahihi, wala kuwajibika kwa usahihi.

     

    Sita, wananchi waendelee kutoa taarifa juu ya upungufu wowote katika eneo la dawa, kwa sababu sauti ya mwananchi ni sehemu muhimu ya kutusaidia kuona ukweli wa hali ilivyo kwenye vituo vya kutolea huduma. Serikali inawataka wananchi waendelee kuwa macho, kutoa taarifa, na kushirikiana nasi katika kulinda ubora wa huduma za afya.

    Serikali itaendelea kuhakikisha kila Mtanzania anapata dawa kwa wakati, kwa ubora unaotakiwa, na kwa utaratibu unaolinda haki yake ya huduma. Hatuwezi kukubali mfumo wenye mianya ya usimamizi, matumizi mabaya ya fedha, takwimu zisizoakisi hali halisi, au upungufu wa uwajibikaji uendelee kumuumiza mwananchi.

     

    Sasa ni wakati wa utekelezaji.Sasa ni wakati wa uwajibikaji.Sasa ni wakati wa matokeo yanayoonekana.

     

    Kila aliyepewa jukumu alitekeleze.Kila mwenye wajibu awajibike. Na kila ngazi isimame kuhakikisha dawa zinapatikana, zinatumika ipasavyo, na zinamfikia mwananchi kama ilivyokusudiwa.

     

    Hiyo ndiyo dhamira ya Serikali. Na hiyo ndiyo kazi tunayokwenda kuisimamia.

     

    Ahsanteni sana.

    |

  • 2 download

    Abstract

    Background: Besides survival and recovery, women afflicted with peripartum cardiomyopathy (PPCM) harbor significant apprehension regarding the safety of future pregnancies. Current knowledge regarding the maternal and fetal outcomes in subsequent pregnancies among women with a history of PPCM is sparse. Likewise, there is insufficient medical evidence to provide guidance for women who opt to become pregnant again after experiencing PPCM.

    Research Questions: What is the feto-maternal prognosis of subsequent pregnancies following a history of PPCM?

    Aims: To describe the fetal and maternal outcomes of subsequent pregnancies following a history of PPCM.

    Methods: We included women from the Tanzania PPCM registry who had subsequent pregnancies after PPCM and assessed PPCM recurrence, maternal prognosis, and fetal outcomes.

    Results: Among the 870 survivors (286 of whom left ventricular function had returned to normal [group 1] and 584 with persistent left ventricular dysfunction [group 2]), subsequent pregnancies were observed in 121 (13.9%) women (78 in group 1 and 43 in group 2). Forty (51.3%) women in group 1 had PPCM relapse, and during a mean follow-up of 896 days, 34 (85.0%) had complete recovery, 3 (7.5%) had persistent heart failure, and 3 (7.5%) died. In group 2, four (9.3%) women had complete recovery, 32 (74.4%) had persistent heart failure, and 7 (16.3%) died. The infant mortality rate was 23.4%.

    Conclusions: After the initial pregnancy complicated by peripartum cardiomyopathy, subsequent pregnancies could lead to PPCM relapse and deleterious feto-maternal outcomes, including death.

    | https://www.ahajournals.org/doi/abs/10.1161/circ.150.suppl_1.4114436

  • 3 download

    Authors: *Naizihijwa G. Majani 1,5 ,  Pilly Chillo 2, Mkiwa Akida3, Judith Lamosai 6, Deogratias Nkya 1,9, Stella Mongella 1, Zawadi, Kalezi 1 Godwin Sharau 8, Vivienne Mlawi 8 , Peter Kisenge, 7, Mohamed Janabi 7, Diederick E. Grobbee 5 , Martijn. G. Slieker 4

    Authors Affiliation:

    1. Department of Pediatric Cardiology, Jakaya Kikwete Cardiac Institute, Dar es Salaam, Tanzania
    2. Department of Internal Medicine, Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS), Dar es Salaam, Tanzania
    3. Department of Pediatrics, Mwananyamala Regional Hospital, Dar es Salaam, Tanzania.
    4. Department of Pediatric Cardiology, Wilhelmina Children’s Hospital, Utrecht, The Netherlands
    5. Julius Global Health, Julius Center for Health Sciences and Primary Care, Utrecht University, Utrecht, The Netherlands
    6. Department of Pediatrics, Muhimbili National Hospital, Dar es Salaam, Tanzania
    7. Department of Adult Cardiology, Jakaya Kikwete Cardiac Institute, Dar es Salaam, Tanzania
    8. Directorate of Surgery, Jakaya Kikwete Cardiac Institute, Dar es Salaam, Tanzania
    9. Department of Pediatrics and Child Health, Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS), Dar es Salaam, Tanzania

    *The corresponding author Naizihijwa G. Majani

    Keywords: Pulse Oximetry, Newborn screening, Neonatal sepsis, Neonatal mortality, Low resource setting.

    Abstract

    Background: Pulse oximetry (POX) is commonly used for early detection of Critical Congenital Heart Disease (CCHD) in newborns, but its potential for identifying other life-threatening conditions in low-resource settings is often overlooked. This study examines the role of POX in detecting conditions beyond CCHD in newborns in Dar es Salaam, Tanzania. 

    Methods: A prospective cohort study was conducted in two Tanzanian hospitals, focusing on identifying CCHD. Pre and post-ductal oxygen saturation (SpO2) readings were taken, and positive screens led to echocardiography evaluations. Newborns with congenital heart disease (CHD) were referred to a cardiac institute, while others were sent to pediatricians for further assessment. Primary outcomes included diagnoses and management strategies for those referred, while secondary outcomes considered hospital stays and survival rates at six months.

    Results: Between October 2020 and June 2023, 10,630 newborns were screened, with 51 (0.46%) testing positive for POX. Of these, 29 (59.2%) were referred to paediatricians, resulting in diagnoses of 10 (34.5%) with sepsis, 10 (34.5%) with transient tachypnea, and 8 (27.6%) with persistent pulmonary hypertension of the newborn. The median hospital stay was 9.2 days (IQR: 7–14 days), and the overall mortality rate was 13.8%, with a six-month survival rate of 86.2%. Newborns diagnosed with sepsis showed the highest mortality. 

    Conclusion: In Tanzania, POX should be utilized as a vital screening tool for both CCHD and other serious neonatal conditions, such as sepsis. Integrating routine POX screening can enable prompt treatment of significant but often asymptomatic conditions in newborns

    |