• P.O Box 65141
  • +255-788-308999

Rais wa Comoro Mhe. Azali Assoumani atembelea kambi ya madaktari bingwa kutoka Tanzania wanaotoa huduma za matibabu katika Kisiwa cha Anjouan

  • Author: JKCI Admin
  • Published At: Wednesday, Oct 08, 2025
image description

Rais wa Comoro Mhe. Azali Assoumani amemshukuru Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwaleta madaktari bingwa kutoa matibabu ya magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa kisiwa cha Anjouan aliyoitoa Julai 6, 2025 katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Comoro.

Akizungumza na timu ya madaktari hao katika hospitali ya Hombo kisiwa cha Anjouan,  Mhe. Rais Assoumani alisema utekelezaji wa ahadi hiyo ni ishara ya undugu na ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.

“Hongereni madaktari kwa kazi nzuri mnayoifanya, sisi wana Comoro tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwaleta ninyi hapa, tunasema asante sana ”, alisema Mhe. Rais Assoumani.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Saidi Yakubu alimweleza Mhe.  Rais Assoumani kuwa wataalam 52 wenye taaluma 17 wameweka kambi ya matibabu kwa siku nane kisiwa cha Anjouan.

“Tunao madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Taasisi ya Kansa ya Ocean Road (ORCI) na Hospitali ya Benjamin Mkapa pamoja na    ” amesema Balozi Yakobu

Mwenyekiti wa Utalii Tiba Taifa Dkt. Peter Kisenge alisema katika kambi hiyo madaktari wanaratajia kuwaona wagonjwa zaidi ya 3,000 waliojisajili na kwamba hadi kufikia jana wagonjwa 1361 wameonwa na madaktari bingwa.