Wagonjwa 2700 watibiwa na JKCI kambi maalumu katika visiwa vya Ngazija Comoro
-
Author: JKCI Admin
-
Published At: Sunday, Jul 06, 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema zaidi ya wagonjwa 2700 wametibiwa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwenye kambi maalumu ya matibabu iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana katika Kisiwa cha Ngazija Visiwani Comoro.
Mhe. Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo wakati akiwahutubia wananchi wa Visiwa hivyo katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Umoja wa Visiwa vya Comoro.
Mhe.Rais Dkt. Samia amesema kwa mwaka wa 2024/2025 wagonjwa zaidi ya 12,000 kutoka Visiwani Comoro walipata huduma mbalimbali za matibabu ya kibingwa nchini Tanzania.
“Kwa mwaka huu wa 2025 kambi maalumu ya tiba ya magonjwa mbalimbali itafanywa na wataalamu kutoka nchini Tanzania katika Kisiwani cha Anjouan, uhusiano uliopo katika sekta ya afya ni wa kuuangalia sana na kuufanyia kazi kwa pamoja”, alisema Mhe.Rais Dkt. Samia.