• P.O Box 65141
  • +255-788-308999

Dkt. Kisenge: Jitokezeni kupima moyo maonesho ya SABASABA

  • Author: JKCI Admin
  • Published At: Sunday, Jul 06, 2025
image description

Wakazi wa Dar es saalam na mikoa ya karibu  wametakiwa  kutembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) lililopo katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) kwaajili ya kupima, kupata elimu, ushauri na kupata matibabu ya moyo .

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es saalam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma wanazozitoa kwenye taasisi hiyo na maonesho hayo kwa kuwahasa wakazi wa Dar es saalamu na mikoa ya karibu waweze kutembelea banda la JKCI ili wapatiwe elimu na matibabu ya moyo na huduma wanazozitoa ikiwemo ya shuka maalumu kwa wagonjwa lijulikananalo kama Dozee.

Dkt. Kisenge ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa moyo  amesema  iwapo mtu atapima afya ya moyo wake mapema itamsaidia kujua  kama ana matatizo au hana, na iwapo anamatatizo itamsaidia kujijua mapema.

“Katika maonesho haya tunatoa tiba ya uchunguzi wa mataibabu ya kibingwa ya magonjwa ya moyo, kwa wale watakaokutwa  na shida ya moyo kwa watoto na watu wazima tutawapa rufaa kutibiwa katika Taasisi yetu, magonjwa ya moyo ni mmoja ya magonjwa yasioambukiza ikiwa watu watafuata mtindo bora wa maisha ikiwemo ulaji wa mboga za majani na matunda kwa wingi”, alisema Dkt. Kisenge.

Dkt. Kisenge pia aliitaja huduma nyingine inayopatikana katika banda hilo ni ile ya teknologia ya kisasa ya kufuatilia hali ya mgonjwa aliyopo nyumbani kwa kutumia teknolojia ya Dozee ambayo inamsaidia Daktari kwa haraka kupata hali halisi ya wagonjwa mara baada ya kufanyiwa upasuaji. Teknologia hiyo ya dozee ambayo ni shuka maalumu inayotandika chini ya kitanda cha mgonjwa inamuwezesha Daktari kujua hali ya upumuaji, presha ya mgonjwa na mapigo ya moyo ya mgonjwa aliyopo nyumbani.

Mwananchi aliyepatiwa huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo katika banda hilo Fortunatus Michael alishukuru kwa huduma ya matibabu aliyopata na kusema kuwa imemsaidia kujua afya ya moyo wake.

“Ninawahamasisha watu waje kutembelea na kupatiwa huduma ya matibabu ya moyo katika banda la JKCI wakati huu wa maonesho ya SABASABA kwani huduma zinatolewa kwa gharama nafuu kuliko ukienda hospitali” alisema Fortunatus

“Nawaomba wananchi wenzangu mje mtembelee banda la Taasisi ya moyo mfanyiwe uchunguzi na matibabu ya moyo kwani gharama ni nafuu ukilinganisha na hospitalini” alisema Fortunatus

Kila mwaka Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imekuwa ikishiriki kwenye maonesho ya sabasaba kwa kutoa huduma za kibigwa za upimaji na matibabu ya moyo ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma hizo.