JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE (JKCI)

National House Corporation leaders go for medical checkup

Viongozi wa mashirika ya Umma na Binafsi wametakiwa kujenga mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara ili kufahamu kama wana magonjwa yanayowasumbua au la na kwa kufanya hivyo wataweza kupata matibabu kwa wakati.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) waliofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya upimaji wa Afya zao.

Prof. Janabi alisema baadhi ya viongozi hawana mazoea ya kupima afya zao japo mara moja kwa mwaka na inapotokea wamegundulika kuwa na tatizo la ugonjwa huwa ni kubwa na limeshaleta madhara mwilini, na wakati mwingine huwa ni vigumu kutibika lakini tatizo kama hilo likigundulika mapema katika hatua ya awali huwa ni rahisi kutibika.

Akizungumzia kuhusu magonjwa ya Moyo Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema ni muhimu mgonjwa afuate maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa aliyopewa na daktari wake kwani kuna baadhi ya wagonjwa wamekuwa na tabia ya kuacha kutumia dawa pindi wanapojiona wamepata naafuu jambo ambalo siyo sahihi.

Akielezea jinsi ya kujikinga na magonjwa ya Moyo kwa upande wa chakula Afisa Lishe kutoka JKCI Louisa Shem alisema ni muhimu kupunguza utumiaji wa vyakula vya mafuta kupita kiasi hasa mafuta yatokananyo na wanyama, kutumia vyakula vya nafaka zisizokobolewa.

Kupunguza unywaji wa pombe na uvutaji wa bidhaa zitokanazo na tumbaku ikiwemo sigara, kufanya mazoezi ya mwili angalau nusu saa kwa siku na kupunguza matumizi ya vyakula vyenye chumvi nyingi.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Afya na Usalama Kazini kutoka NHC Dkt. Yothan Mackenzie alisema hivi karibuni walikuwa na mkutano wa Baraza la Wafanyakazi katika mkutano huo kulikuwa na mada ya ulaji na afya wakaona ni vyema mada hiyo iende sambamba na upimaji wa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Moyo.

Dr. Mackenzie alisema wanawapima viongozi hao kwa awamu hadi sasa jumla ya wakurugenzi na wakuu wa vitengo 14 wamepima na kujuwa afya zao na viongozi wengine wataendelea kupima kwani Shirika lao linaamini kuwa mfanyakazi akiwa na afya njema ataweza kufanya kazi zake vizuri.

Baadhi ya magonjwa waliyopima viongozi hao ni pamoja na Moyo, tezi dume, figo na sukari..

Patient Testimonials

The smiles on their faces show appreciation after successfully surgeries

Happy kids after successfully surgeries

Cardiac Services

Arterial Switch Operation

Arterial Switch Operation

Coronary Angioplasty (PTCA) and Stenting

Coronary Angioplasty (PTCA) and Stenting

Coronary Angiography

The function of coronary arteries is to supply our heart muscle with blood. They may get clogged from a buildup of plaque, cholesterol or cells resulting in..

Coronary Angioplasty

What is Coronary Angioplasty?

Coronary Angioplasty is also known as PCI (Percutaneous Coronary Interventi..

Announcements

On 9th to 19th September 2016, there will be a camp for paediatric open heart surgery at Jakaya K...

We provide several types of clinics public, private and VIP. You are all welcome